USAFIRI WA NDEGE NDANI NA NJE YA NCHI PATA TICKET KIRAHISI
Jinsi ya Kupata Tiketi za Ndege kwenda Tanzania (au kokote) Kwa Gharama Nafuu
Iwapo unasafiri kutoka Kenya au Marekani, tiketi za ndege kwenda Tanzania huwa ni bei kubwa sana na utakuta inachukua kiasi kikubwa ya bajeti yako ya usafiri.
Kwa nini tiketi za ndege zina bei sana?
Kwenye kipindi cha miaka 10, kampuni nyingi za ndege zime filisika au zimejiunga na makampuni mengi. Matokea yake ni kwamba kuna makampuni ya ndege chache zaidi, na hivyo ushindani umepungua na kutoa motisha ya kupunguza bei.
Pia, tangu mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 2001, usalama ndani ya uwanja wa ndege umeongezekea kwa kiasi kikubwa. Na gharama zake nyingi zinalipwa na kodi unayolipa ukinunu tiketi ya ndege.
Hata hivyo, kama unasafiri kwa mara ya kwanza au una uzoefu, hizi vidokezo 5 zitakusaidi kupata tiketi kwa gharama nafuu zaidi.
1. Book mapema
Hii inaonekana kuwa kitu cha urahisi ila wasafiri wengi wana book ticket mwezi moja kabla ya kusafiri, na kampuni za ndege zinajua hili na hivyo huongeza bei ya ticket .
Ila, makampuni ya ndege wanajitahidi kusafiri wakati ndege limejaa. Kwa hiyo, kama safari ya ndege fulani haina watu wengi, watapunguza bei ya tiketi ila kujaza ndege. Vilevile, kama safari ya ndege fulani inatakiwa na watu wengi, wataongeza bei ya tiketi kadri na siku ya kusafiri inavyokaribia.
Kwa kifupi, kama huwezi kubadili tarehe ya kusafiri na umechelewa kubook, utalipa bei yotote utakaopewa. Kwa hiyo, kama itawezekana, book miezi 3 kabla ya kusafiri.
2. Safiri kwenye msimu ambayo watu wengi hawasafiri
Wote tunajua kwamba ndani ya mwaka, kuna wakati ambayo kusafiri kwa ndege ni gharama kubwa. Kwa mfano, ukisafiri kuja Tanzania kati ya Desemba na Februari kutoka nchi inayokumbana na msimu wa baridi. Muda mwingine ni Juni mpaka Agosti, katika kipidi hii family nyingi zinapanga likizo na wanafunzi wa nje wanarudi nyumbani kwa likizo.
Ukiweza kusafiri nje ya misimu kama ya na kusafiri wakati wasafiri sio wengi, utapunguza gharama.
Pia, jaribu kusafiri:
- Katikati ya wiki (Jumanne mpaka alhamisi). Epukana na kusafiri Jumatatu, Ijumaa au Jumapili.
- Asubuhi au usiku sana
Kama kweli unataka kuokoa pesa, tumia prorgamu kama ITA Matrix Airfare Search ambayo itakupa tarehe za kusafiri kwa gharama nafuu kwenda kokote.
3. Tumia kampuni ya Ndege ya Gharama Nafuu
Kama kuokoa pesa ni muhimu zaidi ya kuwa na faraja wakati unasafiri, makampuni ya ndege ya gharama nafuu ndio zakutumia.
- Kama unasafiri kuja Tanzania kutoka Afrika Kusini, Uganda Zimbabwe na Zambia, utaokoa pesa kwa kutumia Fastjet.
- Kama unasafiri kutok Afika Kusini kwenda Zanzibar, jaribu Mango
- Kama unasafiri kutoka Dubai kuja Tanzania, jaribu FlyDubai.
- Pitia kampuni za ndege kwenye orodha yetu ya biashara.
Inawezekana kwamba makampuni ya ndege ya gharama nafuu hayapo kwenye nchi unayotoka au hayaji Tanzania. Sasa, kama ukotayari kutopanda ndege inayokuja Tanazania moja kwa moja, safari kwenda kwenye nchi yenye hizi kampuni za ndege za bei nafuu alafu ipande kutoka hapo. Kwa mfano, kama unasafiri kutoka Ulaya unaweza ukapanda Lufthansa mpaka Dubai alafu ukabadili na kupanda Flydubai mpaka Dar es Salaam.
Ila, kuwa makini na gharama nyongeza, kwa kuwa haya makampuni ya ndege ya gharama nafuu zinabidi zipate faida. Kwa hiyo, hakikisha unasomagharama za mizigo na masharti, bei za chakula n.k.
4. Jiunge na Maili za Wasafiri wa Mara kwa Mara
Huitaji kusafiri mara nyingi sana kutumia maili za wasafiri wa mara kwa mara. Programu ya wasafiri wa mara kwa mara ni programu inayotelewa na kampuni ya ndege ili usipeleke biashara yako kwingine. Kwa kupande ndege ya kampuni hiyo kwa mfululizo, unapewa pointi ambazo zikifikia idadi fulani, itakuwezesha kupata tiketi ya ndege kwa gharama nafuu.
Jinsi unavyozidi kukusanya pointi, utaweza kupunguza gharama yako ya usafiri. Mara nyingine, utajikuta ukisafiri bure.
5. Tumia tovuti bora kubook tiketi yako
Wengi wetu tunavutia na matangazo ya tovuti za kusafiri au makampuni ya ndege yanayoahidi bei za chini. Kwa mfano, ni mara ngapi umejikuta ukiwa umefurahia dili ambayo umekuja kujua kwambo ni punguzoya $0.50 au TZS 1000 tu? Au kwamba hawakuweka kodi na gharama za mizigo?
Kwa hiyo, ni muhimu sana kupitia tovuti nyingi za kusafiri kabla ya kubook tiketi yako, usije ukakosa dili moja ya ukweli. Tovuti bora ni zile zisizokuwa na makubaliano na kampuni moja ya ndege na zina chaguo nyingi za makampuni ya ndege.
Kwa mfano, Travelstart; Ni wakala wa usafiri wa kitanzania na ina kampuni za ndege za kienyeji za nchi nyingi, pamoja na mashirika ya ndege ya kimataifa.
Hakuna nchi kama Tanzania
Kuna sababu nyingi za kusafiri kuja Tanzania kama:
- Utalii
- Safari za kibiashara
- Kutembelea ndugu, jamaa na marafiki
Wakati sababu za kuja Tanzania zinatofautiana, karibia mtu yoyote atakayekuja Tanzania lazima atapapenda pamoja na watu wake. Kwa hiyo, usikubali bei ya tiketi ikuzuie kuja kuona knimacho ya Tanzania. Tumia vidokezo hivi na utaweza kujiapatia tiketi ya bei nafuu kuliko aliyoilipia msafiri mwenzako.
Cha mwisho ni kwamba unaweza kutumia vidokezo hivi ukiwa unapanga safari kwenda kokote kule.
Hakuna maoni: